Tuesday, October 21, 2014

BREAKING NWZZZZ :MSIBA TENA: MSANII SHERRY MAGALI AFARIKI DUNIA!Msanii nyota wa filamu nchini Sherry  Charles Magali akiwa hoi hospitalini Wodi Namba 8 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika picha hii iliyopigwa na mwandishi wetu Ijumaa iliyopita, Okt 17, 2014.

Msanii huyo, amefariki leo saa nne asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa familia, taarifa zaidi za mazishi zitatolewa baadae.Global Publishers imekuwa ikifuatilia hali ya msanii huyu na kuwajulisha mashabiki wake mara kwa mara. Mara ya mwisho kuandika habari zake ilikuwa Februari 21 mwaka huu wakati alipokuwa amelazwa kwenye hospitali Kilimani maeneo ya Big Brother jijini Dar chini ya kichwa

Global Publishers inatoa pole kwa wafiwa na kumtakia marehemu alale pema- ameen!

PICHA 7 ZA KIVAZI CHA AJABU ALICHOTUPIA KIM KARDASHIAN MBELE YA MUMEWE, FULL AIBU MAZEEE

1413748462855_wps_5_Picture_Shows_Kanye_West_PICHA ZAIDI>>>
1413748398504_wps_3_Picture_Shows_Kim_Kardash1413755380026_wps_12_Picture_Shows_Kim_Kardash1413755525861_Image_galleryImage_Picture_Shows_Kim_Kardash1413760725428_wps_56_Junk_food_alert_Kim_Karda1413760806100_wps_57_Junk_food_alert_Kim_Karda

BIBI HARUSI ATOROSHWA!!!

Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.

Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.Akizungumza na chanzo cha habari hizi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lakeliandikwe mtandaoni alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila akimpigia simu hapatikana hewani
Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo..
 Mpaka sasa mama wa bi harusi hajatoa taarifa kwa bwana harusi wala ndugu zake, amekuwa akimtafuta kimyakimya huku akimuomba Mungu binti yake apatikane kwa vile mahari  alishalipwa, sasa anaogopa ikifika siku ya ndoa itakuwa aibu kubwa
alisema ndugu huyo.
Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.

Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu;  BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.

LINAH, MCHUMBA’KE WATIBUANA!MCHELE ulionyooka! Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’ na mchumba’ke, Nangari Kombo wanadaiwa kutibuana, kisa kikidaiwa ni maneno ya wanafiki yasiyokuwa na ukweli.
Staa wa Bongo Fleva, mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Estelina Sanga ‘Linah’
Habari za chini ya kapeti zilinyetisha kwamba mtiti kati ya wawili hao ulijiri juzikati baada ya Kombo kudaiwa kuanza kumtuhumu Linah kuwa anapokuwa kwenye ziara za matamasha kama Fiesta huwa anamsaliti na wanaume wengine.
 
Lina akiwa na mpenzi wake, Nangari Kombo.
Chanzo hicho kilidai kwamba, kufuatia madai hayo Kombo alimuanzishia Linah bonge la tafrani na kujikuta kila mmoja anachukua hamsini zake.
Linah alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Ni kweli kulitokea kutoelewana but (lakini) tumeyamaliza, tupo vizuri sana.”

Monday, October 20, 2014

DIDA AZIKA RASMI NDOTO ZA KUOLEWA

Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’.

NDOA basi! Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai kuwa, amebaini kujiingiza kwenye ulimwengu huo ni kujipa ‘stress’ za kujitakia. 

PATAMU: KADINDA AMFUATA JACK PATRICK GEREZANI

Martin Kadinda wakati  akiwa na Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Stori: Mayasa Mariwata
Imekaa poa sana! Ubuyu kutoka Hong Kong, China unadai kwamba mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda hivi karibuni alimfuata Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani aliyefungwa nchini humo kwa msala wa kukamatwa na madawa ya kulevya. Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Isaac Sepetu zilidai kwamba katika safari yake nchini humo, alifuatana na Wema na Petit Man

Mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda akipozi.
“Kadinda amepongezwa sana kwa hatua yake hiyo, kuhusu kama alionana naye au alichoongea naye, tusubiri arudi maana bado yupo China,” alisema rafiki wa mmiliki huyo wa lebo za mavazi za Single Button na Kwachukwachu.

Sunday, October 19, 2014

LIBEBEKE JIPYA LA UDAKU


NOMA SANA MAZA WA MAKAMU AVUA NGUO BAADA YA KUSINGIZIWA KUIBA SIMU YA NOKIA TOCHI


Mwanamke mmoja (pichani) aliyedaiwa kuwa ni mke wa mtu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya mwaka baada ya kutuhumiwa kwa wizi wa simu ya mkononi kwenye harusiniTimbwili hilo lililoshuhudiwa na mpiga chabo wetu lilimkuta mwanamama huyo ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza. Baada ya kusingiziwa mmama huyu aliamua chojoa nguo zote mbele ya walizi ili ili kuthibitisha kuwa hakuichukua.

Saturday, October 18, 2014

MAKAVU LIVE: ‘JACQUELINE WOLPER APIME UKIMWI’

MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amemtaka msanii mwenzake, Jacqueline Wolper apime Ukimwi kama alivyofanya yeye. 

Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’. Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema anamheshimu Wolper na kamwe hawezi kumsema vibaya lakini alishangaa kuambiwa na mashosti wake kwamba anamsema yeye ana Ukimwi. “Nilishangaa sana kwa kweli hilo jambo liliniumiza roho na linaniuma mpaka kesho, eti anawaambia watu mimi ni muathirika, lini alinipima au ana uthibitisho gani na hilo,” alisema Rayuu na kuongeza:
“Kutokana na kunikosesha raha kwa kiasi kikubwa kwa jambo hilo, niliangua kilio nikaamua kwenda kupima na kuyaanika majibu yangu kwenye Istagram ili aumbuke kwa kuwa nipo safi, kama na yeye anaweza, akapime tuone majibu yake.”
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper. Kutokana na mtafaruku huo, mapaparazi wetu walifanya juhudi za kumsaka Wolper pasipo kuzaa matunda, ambapo simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wenye mlolongo mzima wa ishu hiyo, hakujibu.
 
Top